BAGHDAD:watu 27 zaidi waangamia nchini Irak
23 Agosti 2007Matangazo
Watu wasiopungua 27 wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye mji wa Beiji kaskazini mwa Irak.
Watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulio hilo ambapo mshambuliaji alilitosa lori lake katika kituo cha polisi na kulipua mabomu.
Habari zaidi zinasema kuwa wengi wa waliouawa walikuwa raia.
Wakati huo huo askari 14 wa Marekani wameuawa baada ya helikpota yao kuanguka kaskazini mwa Irak.