1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Waziri Mkuu Nuri Maliki ajitetea

15 Julai 2007

Waziri Mkuu wa Irak bwana Nuri al Maliki amepinga lawama zinazotolewa dhidi ya serikali yake na amejitetea kwa kusema kuwa mazingira ya kivita ndiyo yanayochelewesha utekelezaji wa malengo yanayokusudiwa na serikali yake.

Bwana Maliki ameeleza kuwa ujiingizaji kutoka nje pia unachangia katika mazingira hayo.Waziri mkuu huyo pia ameitaka Mrekani impe muda zaidi ili aweze kufikia malengo yanayokusudiwa.

Hilo ni tamko la kwanza la waziri mkuu Maliki tokea Marekani itoe ripoti yake juu ya hali ya sasa nchini Irak.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW