Baibui linavyopoteza maana yake
27 Agosti 2014Matangazo
Ni bahati mbaya sana kwamba jamii hujikuza zikilazimika kuachilia tamaduni na mila zake kupotea, mambo ambayo ni muhimu sana kwa utambulisho wake kama jamii fulani. Katika makala hii ya Utamaduni na Sanaa, Amina Abubakar anaangazia kwa undani zaidi vazi lililotumiwa sana na wanawake wa Kiswahili kujistiri, buibui la ukaja au buibui la jadi la Kiswahili kama linavyojulikana na wengi.
Swali kubwa analouliza kwenye makala hii ni iwapo kutekwa kwake na mabuibui ya kisasa ni sawa na kuutupa utamaduni wa Kiswahili au muonekano wa asili ya mwanamke wa Kiswahili!
Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Khelef