Baidoa, Somalia. Waziri auwawa.
29 Julai 2006Matangazo
Watu wenye silaha wamempiga risasi na kumuua waziri mmoja wa Somalia nje ya msikiti mjini Baidoa jana Ijumaa.
Kuuwawa kwa waziri huyo wa katiba na utawala wa majimbo Abdallah Isaq Deerow kulizusha machafuko mjini Baidoa ambako ni makao makuu ya serikali hiyo.
Wakati huo huo kuna wasi wasi kuwa wapiganaji wa muungano wa baraza la mahakama za Kiislamu wanapata silaha kwa siri , baada ya ndege kutua katika uwanja wa ndege wa Mogadishu, ikiwa ni mara ya tatu tangu kufunguliwa kwa uwanja huo hivi karibuni.
Serikali ya Somalia inaishutumu Eritrea kwa kuwapa kwa siri silaha wapiganaji hao wa Kiislamu.