1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bajeti kuu Kenya yagonga sh. 3.3 Trilion

Shisia Wasilwa
7 Aprili 2022

Waziri wa Fedha wa Kenya Ukur Yattani leo amewasilisha Bungeni bajeti ya serikali yenye kima cha shilingi trilioni 3.3 za Kenya kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

Uhuru Kenyatta Präsident Kenia Rede Parlament Nairobi
Picha: Simon Maina/AFP via Getty Images

 Bajeti hiyo iliyozingatia ajenda nne kuu za serikali, ina nakisi ya shilingi bilioni 846, zitakazofidiwa kwa mikopo na msaada kutoka kwa wahisani.

Serikali kuu imepata mgao mkubwa kwenye bajeti hii ambayo ni ya mwisho kusomwa chini ya utawala wa Rais Uhuru Kenyatta, ikitengewa shilingi trilioni 2.07. Ofisi ya rais imepokea shilingi trilioni 2.01, Bunge limetengewa shilingi bilioni 38.4.

Soma zaidi:Kenya: Viongozi watoa wito wa kuvumiliana kisiasa

Idara ya mahakama imetengewa shilingi bilioni 18.8. Serikali za majimbo zimetengewa shilingi bilioni 370. Kufuatia uhaba wa mafuta ambao umekuwa ukishuhudiwa nchini kwa kipindi cha juma moja sasa, serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 24.7, ili kuwasaidia wananchi dhidi ya nyongeza ya bei za mafuta.

Ili kujaza sehemu ya nakisi kwenye bajeti, mkenya atahitaji kulipa kodi ya shilingi bilioni 570, huku serikali ikitarajiwa kukopa shilingi bilioni 270 kwa washirika wafadhili.

Bajeti yapaa ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita

Ukur Yatani alianza kusoma bajeti ya taifa mwendo wa saa tisa alasiri asimilia 4.8 zaidi ikilinganishwa na bajeti iliyopita ya shilingi trilioni 2.9. Kampuni za kuagiza dawa zimeondolewa kodi za dawa.

Waziri wa fedha ameliambia bunge kwamba bajeti hiyo kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023, inalengo la kufufua uchumi wa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Raia wa KenyaPicha: Dai Kurokawa/epa/dpa/picture alliance

Ameongeza mbali na mambo mengine, bajeti imebeba ajenga kuu nne ikiwemo kuhakikisha maisha bora kwa wakenya "mapendekezo ya bajeti mwaka huu 2022/2023 ni shilingi trilioni 3.3"

Soma zaidi:Mtandao umeviwezesha vitongoji maskini nchini Kenya

Bajeti yenyewe imesomwa huku mwananchi akizidi kubanwa na ongezeko la gharama ya maisha, uhaba wa mafuta, athari za janga la Covid 19, katika mazingira ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika mwezi wa nane kwa mujibu wa katiba.

 

Kibarua kizito cha deni la taifa  kwa Rais ajae Kenya

Mrithi wa Rais Uhuru Kenyatta, atahitaji kutumia wastani wa shilingi bilioni tatu kila siku kulipia madeniambayo yameuzonga utawala wa serikali ya Jubilee, ambayo yamezidisha kiwango cha kukopa fedha katika mashirika ya fedha ulimwenguni.

Wataalamu wanasema kuwa kwa kila pato la shilingi 10 kwa serikali, shilingi sita zitakuwa zinalipa madeni hayo ambayo ambayo yamefikia shilingi trilioni 8.2.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliitafsiri makadirio hayo ya bajeti hayajamuangalia mwananchi wa kawaida, kutokana na kushuhudiwa kwa makali ya maisha, kupanda bei kwa bidhaa muhimu.

Kodi ya matangazo katika vyombo vya habari kwa mchezo ya kamari imeongezwa kwa asilimia 15 sawa na bidhaa za za tumbaku. Bajeti ya mwaka huu.

Soma zaidi:Kenya kutupa dozi 800,000 za Covid-19 zilizoisha muda

 imesomwa miezi miwili mapema ili kutoa muda mwafaka kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu ulioratibiwa  kufanyika tarehe nane mwezi wa nane mwaka huu.

Kwa kawaida bajeti husomwa mwezi wa sita kila mwaka. Mfumko wa bei kwa sasa ni asilimia 5.6. Bunge sasa linatarajiwa kuyajadili mapendekezo hayo kabla ya kuidhinishwa na Rais.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW