Bajeti ya Msaada wa Maendeleo kupungua
21 Novemba 2012Wakati Dirk Niebel alipoingia mwaka 2009 kama waziri wa ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi nchini Ujerumani aliikuta bajeti ya wizara hiyo ikiwa ni Euro Billioni 5.8.Katika miaka iliyofuata chama cha FDP ambacho ni mshirika katika serikali kuu ya Ujerumani kilipata nafasi nzuri ya kufurahia kiwango cha bajeti kubwa katika wizara hiyo ambacho kilifikia yuro Billioni 6.4 hadi hivi sasa.
Mchango rasmi wa serikali katika wizara hiyo ambayo inahusika na misaada ya maendeleo ulionekana kuongezeka hadi mwaka huu wa 2012 ambapo kiwango hicho kilipunguzwa kutoka asilimia 0.35 hadi asilimia.04 ya pato la ndani. Wakati wa bajeti ya wizara hiyo kupanda umekwisha na kinachodhihirika ni kwamba wizara ya maendeleo sasa kukabiliana na punguzo zaidi la hadi Euro Milioni 87.
kupunguzwa kwa bajeti hiyo ni dhamana ya makundi yaliyomo serikali katika bunge la Ujerumani. Kutokana na wingi wao bungeni wangeweza kuibadili hatua hiyo katika muda wa chini ya wiki mbili na kuupitisha muswaada wa serikali , unaotaka bajeti ya wizara hiyo ya misaada ya maendeleo iongezwe kwa Yuro 38. Kundi la wabunge kutoka upande wa chama cha waziri Dirk Niebel FDP na washirika wake wahafidhina vyama ndugu vya CDU/CSU vilihalalisha uamuzi wake bila ya kuzingatia mpango wa maendeleo wa Umoja wa Ulaya.
Waziri Niebel ameghadhabishwa na kuvunjwa moyo na hatua hiyo,na kutokana na hilo sasa itabidi waziri huyo katika mwaka 2013 aiendeshe wizara yake na bajeti ndogo kabisa.Miradi mbali mbali pamoja na taasisi husika zitajikuta zikikabiliwa na matatizo ikiwemo zile za Umoja wa Ulaya.Niebel amesikitishwa sana na hali hii lakini lawama zote zinabebeshwa chama chake na washirika wake katika serikali ya muungano.Akizungumza kwa masikitiko makubwa Niebel amesema bunge limetoa umuhimu katika masuala mengine katika Bajeti ya mwaka 2013 kuliko yale yaliyopendekezwa na serikali na hilo halina budi kuridhiwa.
Kughadhabishwa kwa Niebel kunatokana na wasiwasi uliopo hasa baada ya bunge kutaka itengwe asilimia 0.7 ya kiwango jumla cha pato la ndani kwa ajili ya kushughulikia shughuli zote za misaada ya maendeleo hadi alau mwaka 2015 jambo ambalo hata Niebel mwenyewe akifahamu fika haliwezekani.Itakumbukwa kwamba tangu mwaka 1970 hakuna serikali yoyote ya ujerumani iliyoweza kufikia kiwango hicho,lakini kiwango bora kabisa kuwahi kufikiwa ni katika miaka ya 1980 ambapo kilifikia 0.47 asilimia.
Tatizo katika suala zima ni kukosekana nia ya kisiasa.Tangu Umoja wa Mataifa ulipotangaza malengo ya maendeleo ya Milenium hakuna juhudi zinazoonekana kufanikiwa linapokuja suala hili yote ni kwasababu nia ya kisiasa haipo .
Sambamba na hayo katika bunge la Ujerumani Bundestag kulifikiwa uamuzi kwa wingi wa kura,kuhusu kiwango cha 0.7 asilimia . Mnamo mwezi Februari 2011, wabunge kutoka vyama vyote vitano bungeni walitoa wito kutaka lengo hilo la 0.7 asilimia libakie kama lilivyo.
Wabunge 372 kati ya 622 wanaunga mkono ongezeko la kila mwaka katika bajeti ya msaada wa serikali, kwa alau euro bilioni 1.2 ifikapo 2015. Kimsingi ni kuwa karibu 60 asili mia awanaunga mkono.
Lakini huenda chama cha kijani pindi kitapata matokeo mazuri katika uchaguzi mkuu 2013 na hivyo kuunda serikali ya muungano na SPD kikabadili uamuzi huo. Shirika la misaada la Welthungerhilfe na lile la kuwasaidia watoto la "Terre des Hommes", yanasema kupunguza msaada kutatoa ishara mbaya, katika wakati ambapo Ujerumani inakabiliwa na changamoto mpya, mabadiliko ya tabia nchi, uhamiaji na upungufu wa rasili mali. Mkuu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali "Venro" Ulrich Post anasema kwa kufanya hivyo sura na hali ya kuaminika ya serikali ya Shrikisho katika nchi za nje itatoweka.
Mwandishi: Fürstenau,Marcel/ Saumu Yusuf
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman