Bajeti ziada yaidhinishwa na bunge la Ujerumani:
26 Novemba 2003Matangazo
BERLIN: Wakati pakisikika lawama kuhusika na nakisi ya bajeti ya Ujerumani, serikali ya muungano ya kansela Gerhard Schroeder imetumia wingi wake bungeni kuidhinisha bajeti ziada kwa ajili ya mwaka huu. Mikopo mipya imepanda hadi EURO billioni 43, na hii ni rikodi kufuatia vita vya pili vya dunia, na ni zaidi ya billioni 19 kuliko ilivyoandaliwa na waziri wa fedha Hans Eichel. Upinzani wa wahafidhina ulipinga kudurusiwa upya bajeti, na ulisema inakiuka kiwango kilichotajwa na katiba ya Ujerumani. Benki Kuu ya Ulaya imetaja uamuzi huo unaweza kuhatarisha sera za fedha za Muungano wa Ulaya.