Balaa la Wakimbizi wa Kiafrika Mediterania
12 Mei 2015Umoja wa Mataifa Jumatatu (11.05.2015) uliarifiwa kuhusu janga la wahamiaji katika bahari ya Mediterenia na mapendekezo yatakayowalenga wafanyabisahara haramu ya kusafirisha binadamu wanaozidi kuuchochea mzozo huo.
Kuokolewa kwa watu hao, thuluthi moja kati yao wakiwa wanawake, ambao watatu walikuwa wajawazito, ni tukio la hivi karibuni la kuokolewa maelfu ya wakimbizi wanaojaribu kuingia Ulaya kutumia boti za walanguzi. Wengi wao wamekuwa wakianzia safari yao kutoka pwani ya Libya, ambako wafanyabiashara ya kusafirisha binadamu wamekuwa wakiendesha shughuli zao bila hofu ya kukamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote kisheria na wakiutumia mzozo wa kisiasa na machafuko yanayoendelea nchini humo.
Katika kipindi chetu cha Maoni Mbele ya Meza ya Duara leo tunajadili suala la wakimbizi wa kiafrika kukimbia nchi zao na kujaribu kuingia Ulaya kutafuta maisha mazuri na maafa yanayoshuhudiwa katika bahari ya Mediterania na katika pwani ya Italia. Mwenyekiti ni Josephat Charo.
Kusikiliza kipindi bonyeza alama ya spika hapo chini.
Mwandishi:Josephat Charo
Mhariri:Daniel Gakuba