1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Balozi wa Afrika Kusini aliyekutwa amekufa aliacha ujumbe

1 Oktoba 2025

Ofisi ya mwendesha mashtaka mjini Paris imesema Balozi wa Afrika Kusini nchini Ufaransa, aliyekutwa amekufa katika hoteli ya Hyatt Regency mjini Paris jana Jumanne, alimuachia mkewe barua ya kujitoa muhanga.

Afrika Kusini Johannesburg 2021 | Mkutano na waandishi wa habari wa Rais wa CAF na Waziri wa Michezo Nathi Mthethwa
Kabla ya kuchaguliwa kuwa balozi, Mthethwa alishika nyadhifa mbalimbali za ngazi za juu kwenye serikali ya Afrika KusiniPicha: Gavin Barker/Sports Inc/empics/picture alliance

Mwili wa Balozi Nkosinathi Emmanuel Mthethwa iligunduliwa na mlinzi jana asubuhi kwenye ua wa ndani wa hoteli hiyo magharibi mwa Paris, alikokodisha chumba kwenye ghorofa ya 22.

Jumatatu jioni mkewe aliwaarifu polisi kwamba hajui mumewe aliko baada ya kupokea ujumbe ambao alimuomba msamaha na kumuelezea nia yake ya kujiua.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa balozi huyo alinuia kuchukua hatua hiyo na hakusaidiwa na yoyote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW