1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Lambsdorff: Urusi haina mpango wa mazungumzo ya amani

17 Agosti 2024

Balozi wa Ujerumani nchini Urusi Alexander Graf Lambsdorff amesema Moscow haiko tayari kufanya makubaliano ya amani na Ukraine.

Urusi | Balozi wa Ujerumani, Alexander Lambsdorff
Balozi wa Ujerumani nchini Urusi Alexander Lambsdorff asema Urusi haina mpango wa mazungumzo ya amani na UkrainePicha: Vyacheslav Prokofyev/TASS/dpa/picture alliance

Balozi Lambsdorff amesema hayo alipozungumza na gazeti la Ujerumani la General-Anzeiger.

Amesema, masharti ambayo Rais Vladimir Putin amekuwa akiyasisitiza kabla ya mazungumzo ambayo ni pamoja na kuitaka Ukraine kuondoka kabisa kwenye maeneo ambayo anaamini wanayadhibiti, yanaashiria kabisa kwamba hana mpango wa kujadiliana.

Amezungumzia pia mafanikio ya mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya Ukraine katika jimbo la Kursk akisema ni wazi yameipa kiwewe Urusi na hasa kwa kuwa yalikuwa ya kushtukiza. 

Na alipozungumzia mabadilishano makubwa ya wafungwa kati ya Urusi na mataifa ya magharibi, balozi huyo amesema hayakuashiria kuimarika kwa mawasiliano na Moscow, kwa kuwa Putin hakua na kingine zaidi ya wasiwasi juu ya Krasikov, aliyefungwa Ujerumani baada ya kukutwa na hatia ya mauaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW