1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Balozi wa Ujerumani yuko Moscow kwa mazungumzo, siyo kuitwa

4 Machi 2024

Balozi wa Ujerumani nchini Urusi, Alexander Graf Lambsdorff, alifanya mazungumzo, kwenye wizara ya mambo ya nje ya Urusi juu ya masuala ya nchi mbili hizo.

Urusi Moscow | Balozi wa Ujerumani Moscow Alexander Graf Lambsdorff
Balozi wa Ujerumani Moscow Alexander Graf LambsdorffPicha: Sergei Bobylev/TASS/IMAGO

Balozi Lambsdorf ameeleza kuwa alipata mwaliko wa kujadili masuala mbalimbali yanayozihusu Ujerumani na Urusi.

jerumani pia imeeleza wazi kwamba balozi Lambsdorf alihudhuria mazungumzo yaliyopangwa muda mrefu uliopita na kwamba hayahusiani na mkasa wa kuvuja kwa mazungumzo yaliyodukuliwa ya wanajeshi wa Ujerumani juu ya uwezekano wa kuyapeleka makombora ya Taurus nchini Ukraine.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, amesema mazungumzo hayo yanadhihirisha kwamba nchi za Magharibi zinajihusisha moja kwa moja kwenye vita vya Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW