1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAMAKO: Rais Chavez wa Venezuela ziarani Mali

2 Agosti 2006

Rais Hugo Chavez wa Venezuela hii leo anafanya ziara fupi nchini Mali yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Chavez anatazamia kukutana na rais wa Mali Amadou Toumani Toure kabla ya kuelekea Benin.Mali na Venezuela mwaka 2003 zilitia saini hati iliyoeleza matarajio ya Venezuela kuipatia Mali petroli na Venezuela kununua zao la pamba moja kwa moja kutoka Mali.Mwezi mmoja uliopita katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika nchini Gambia,rais Chavez alitoa mwito kwa viongozi wa Kiafrika waungane na Amerika ya Kusini kushirikiana hasa katika sekta ya mafuta na shughuli za benki ili kujiepusha na kile alichokiita “utawala wa kigeni”.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW