BAMAKO : Rais Toure wa Mali achaguliwa tena
4 Mei 2007Rais Amadou Toumali Toure wa Mali amechaguliwa tena kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliopita.
Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliotangazwa jana Tuore amejizolea asilimia 68.3 ya kura wakati mpinzani wake mkuu Ibrahim Boubacar Keita amejipatia asilimia 18.6.
Wafuasi wa Keita,spika wa bunge na waziri wa mkuu wa zamani wamerudia tena nia yao ya kupinga matokeo hayo na wametaka kubatilishwa kwa matokeo hayo ambayo wamesema kuwa hawayatambui kwa sababu ni upuuzi kwa uchaguzi huo.
Waangalizi wa kigeni na wanadiplomasia wanasema kumekuwepo na matatizo machache ya kiufundi wakati wa uchaguzi huo katika koloni hilo la zamani la Ufaransa mojawapo ya nchi maskini kabisa duniani lakini kwa ujumla uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na wa kuaminika.