Bandari za EU zaungana dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya
25 Januari 2024Matangazo
Uzinduzi wa muungano huo uliofanyika katika bandari ya Antwerp nchini Ubelgiji, lango kuu la uingizaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine barani Ulaya, ulihudhuriwa na mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya na wawakilishi kutoka bandari 16 za umoja huo, pamoja na mashirika ya usafiri wa baharini.
Muungano unahitajika kukabiliana na wahalifu
Kamishna wa mambo ya ndani katika Umoja wa Ulaya Ylva Johansson, amesema kwamba wanahitaji kuwa na muungano huo ili kukabiliana na mtandao huo wa wahalifu.
Bandari kuu za Ulaya zimekumbwa na ghasia kutoka kwa makundi ya mafia wa maeneo hayo walioazimia kudumisha biashara hiyo haramu yenye faida kubwa kwa njia yoyote ile.