1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Banghladesh yamuachia huru kiongozi wa chama cha kiislamu

12 Machi 2024

Baada ya miezi 15 tangu maafisa wa kupambana na ugaidi walipomkamata wakati alipoapa kushiriki maandamano ya kuipinga serikali.

Polisi wamuachilia kiongozi wa chama kikubwa cha kiislamu nchini Bangladesh
Polisi wamuachilia kiongozi wa chama kikubwa cha kiislamu nchini BangladeshPicha: Khairul Alam Foysal/DW

Serikali ya Bangladesh imemuachilia huru kiongozi wa chama kikubwa cha kiislamu, miezi 15 tangu maafisa wa kupambana na ugaidi walipomkamata wakati alipoapa kushiriki maandamano ya kuipinga serikali.

Kuachiwa huru kwa mkuu wa chama cha Jamaat-e-Islami, Shafiqur Rahman, kunakuja wakati msuguano wa kisiasa ukipungua kufuatia ushindi wa nne mfululizo wa waziri mkuu Sheikh Hasina mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Msemaji wa chama Matiur Akanda ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Rahman, mwenye umri wa miaka 65, aliachiliwa huru kutoka gereza lenye ulinzi mkali nje ya mji mkuu Dhaka jana Jumatatu, saa chache kabla ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani kuanza katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya waislamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW