BANGKOK:Ibrahim Gambari ziarani Asia mashariki
15 Oktoba 2007Matangazo
Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa anaeshughulikia mgogoro wa kisiasa nchini Myanmar Ibrahim Gambari ameanza ziara ya nchi za kusini mashariki mwa Asia.
Katika kituo cha kwanza cha ziara hiyo bwana Ibrahim Gambari amefanya maungumzo na viongozi wa Thailand.
Lengo la ziara yake ni kuzishawishi serikali za nchi hizo ziunge mkono hatua kali dhidi ya utawala wa Myanmar uliotumia nguvu kuzima upinzani wa watetezi wa demokrasia nchini humo.
Mjumbe huyo anatarajiwa kuenda Myanmar baada ya kuzitembelea Malyasia, Indoneshia, Japan na China.
Wakati huo huo wapinzani wengine sita walikamatwa mwishoni mwa wiki nchini Myanmar.