1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAsia

Bangladesh bado haina huduma ya Internet kufuatia machafuko

22 Julai 2024

Huduma ya mawasiliano ya Intaneti imeendelea kuzimwa nchini Bangladesh kwa siku ya tano mfululizo huku serikali ikitangaza leo kuwa siku ya mapumziko.

Jeshi likiwa kwenye doria kwenye mji mkuu wa Dhaka.
Jeshi likiwa kwenye doria kwenye mji mkuu wa Dhaka.Picha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Mamlaka za nchi hiyo zimeendelea kudhibiti hali ya usalama licha ya kurejea utulivu kiasi baada ya mahakama kutowa amri ya kuondolewa mfumo wenye utata wa kugawa nafasi za ajira za serikali,na ambao ulichochea maandamano makubwa ya vurugu nchini Bangladesh.  

Kwa siku kadhaa nchi hiyo iko chini ya amri inayokataza watu kutembea nje na wanajeshi wamekuwa wakionekana wakipiga doria katika mji mkuu na maeneo mengine.

Soma pia:Babladesh: Kiongozi wa maandamano ahofia usalama wake

Machafuko makubwa yameshuhudiwa kati ya polisi na waandamanaji wengi wanafunzi wanaotaka uondolewe mfumo unaotenga asilimia 30 ya ajira za serikali, kwa kwaajili ya familia za wanajeshi wakongwe waliopigana vita vya kudai Uhuru wa Bangladesh mwaka 1971.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW