Bangladesh yafutilia mbali vipengee vya upendeleo vya kazi
21 Julai 2024Mahakama ya Juu ya Bangladesh imefuta sehemu kubwa ya vipengele vya upendeleo kwenye kazi za serikali, ambavyo viliibua maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi.
Kitengo cha Rufaa cha mahakama hiyo kilitupilia mbali amri ya mahakama ya chini ambayo ilikuwa imerejesha kanuni za upendeleo, na kuelekeza kuwa asilimia 93 ya kazi za serikali zitakuwa wazi kwa watu kuziomba kwa kuzingatia sifa na bila upendeleo.
Soma pia: Jeshi la Bangladesh laingia mtaani kuwadhibiti waandamanaji
Serikali ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina ilikuwa imetupilia mbali mfumo wa upendeleo katika kazi za serikali mwaka wa 2018, lakini mahakama ya chini iliurudisha na kuibua maandamano ya vurugu na kusababisha vifo vya takriban watu 114 katika taifa hilo la Asia Kusini. Chini ya kanuni hizo zilizozusha maandamano, asilimia 30 za kazi zote za serikali zilikuwa kwa ndugu na jamaa wa wanajeshi waliopigana vita vya ukombozi wa Bangladesh vya mwaka 1971.