1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangladesh yaitaka India kumrejesha Hasina nyumbani

17 Novemba 2025

Bangladesh imeitolea mwito India kumrejesha nyumbani Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina, pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Asaduzzaman Khan Kamal, baada ya kuhukumiwa kifo.

 Dhaka 2024 | Sheikh Hasina
Waziri Mkuu wa zamani Bangladesh Sheikh HasinaPicha: Indranil Mukherjee/AFP

Wawili hao walikutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuamuru kuandamwa kwa waandamanaji vijana mwaka uliopita waliokuwa wanadai mabadiliko nchini humo.

Nchi hiyo imesema India ina jukumu la kufanya hivyo chini ya makubaliano ya  kuwarejesha nyumbani watu waliohukumiwa nchini mwao wakati wakiwa uhamishoni.

Hasina na mwenzake waliiitoroka nchi wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z, mwaka uliopita na tangu mwezi Agosti mwaka huo wamekuwa wakiishi katika nchi hiyo jirani.

Maandamano hayo yaliyosababisha mauaji ya zaidi ya watu 800 huku wengine zaidi ya 14,000 kujeruhiwa,  yalichangia kuanguka kwa utawala wa Hasina wa miaka 15. Mwezi Fenruari mwaka huu Umoja wa Mataifa ilitoa ripoti iliyosema idadi ya waliouwawa Bangladesh kufuatia vurugu za maandamano ilifikia 1,400.

Hukumu dhidi ya Sheikh Hasina  imekuja miezi kadhaa kabla ya uchaguzi wa bunge wa Februari mwakani. Chama cha Hasina cha Awami kimepigwa marufuku ya kushiriki uchaguzi huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW