SiasaBangladesh
Bangladesh yasema haina mipango ya kukizuia chama cha Hasina
12 Agosti 2024Matangazo
Tamko hilo limetolewa hii leo na waziri mpya wa mambo ya ndani wa Bangladesh, Sakhawat Hossain. Amewaambia waandishi habari kuwa serikali mpya haipuuzi mchango mkubwa uliotolewa na chama cha Hasina kwa taifa hilo na kwamba uchaguzi utakapoitishwa kitaruhusiwa kushiriki.
Soma pia: Muhammad Yunus atoa wito wa kuungana kuijenga upya Bangladesh
Katika hatua nyingine, polisi ya nchi hiyo imeanza tena kutekeleza majukumu yake ya kusimamia usalama baada ya wiki nzima ya mparaganyiko kufuatia hatua ya kujiuzulu kwa Hasina.
Maafisa wa polisi wameonekana wakishika doria kwenye mji mkuu, Dhaka, wiki moja tangu wimbi la maandamano ya vijana kumlazimisha Hasina kuachia ngazi na kuikimbia nchi hiyo.