BANGUI Vita dhidi ya rushwa
22 Septemba 2005Matangazo
Asasi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNDP kwa kushirikiana na jopo la kimataifa Transparency international linakusudia kuanza uchunguzi juu ya kuenea kwa rushwa katika jamhuri ya Afrika ya Kati.
Uchunguzi huo unatarajiwa kuanza leo kwa ridhaa ya serikali ya nch hiyo.
Rushwa imekuwa kipingamizi kikubwa katika maendeleo ya nchi hiyo.Tokea kuchaguliwa kwake kwa njia za kidemokrasi mwezi mei mwaka jana, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amechukua hatua thabiti ikiwa pamoja na kuunda kamati za kuchunguza rushwa nchini.