1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANJUL: Wa-Gambia wapiga kura kumchagua rais

22 Septemba 2006
Wa-Gambia hii leo wanapiga kura kumchagua rais wa nchi yao.Yahya Jammeh alienyakua madaraka bila ya kumwaga damu miaka 12 iliyopita,anagombea kubakia na wadhifa wa rais kwa mara ya tatu.Jammeh mwenye umri wa miaka 41 anapambana na mwanasheria mashuhuri anaetetea haki za binadamu,Ousainou Darboe alie na miaka 58 na vile vile mwanasiasa mwengine,Halifa Sallah mwenye umri wa miaka 53.Kiasi ya wapiga kura 670,336 wameandikishwa kupiga kura zao katika vituo 989 sehemu mbali mbali za nchi.Matokeo ya uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa mapema siku ya Jumamosi.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW