1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Baraza Kuu UN lataka amani, vita visitishwe haraka Ukraine

25 Februari 2026

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha Jumanne azimio lake linalotoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano yanayoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Vita hivyo vilianza mwaka 2022 Urusi ilipoivamia Ukraine.

 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York 2026
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena BaerbockPicha: Bianca Otero/ZUMA/IMAGO

Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalotaka pia amani ya kudumu ya Ukraine na kuheshimu sheria za kimataifa, limepitishwa Jumanne ikiwa ni miaka minne tangu Moscow ilipoivamia Ukraine.

Marekani yasita kupiga kura kuliunga mkono azimio

Mataifa 107 wanachama wa Umoja wa Mataifa yalipigia kura ya kuunga mkono azimio hilo wakati 12 yamepinga. Nchi 51 hazikupiga kura ya kulikataa au kuliunga mkono ikiwemo Marekani.

Rais wa Baraza Kuu la umoja huo Annalena Baerbock ameizungumzia hatua hiyo na kusisitiza kuwa amani itapatikana na kuwa ya kudumu  kama itazingatia kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuheshimu uhuru wa Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW