1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Urusi laridhia unyakuzi wa majimbo 4 ya Ukraine

4 Oktoba 2022

Bunge la Urusi limepigia kura idhinisho la kuijumuisha mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Urusi, hatua inayoonesha wazi nia ya serikali ya taifa hilo kujinyakulia rasmi maeneo hayo katika kipindi cha miezi 7 ya vita

Russland Moskau | Parlament
Picha: Sergei Fadeichev/TASS/dpa/picture alliance

Katika kikao cha Jumanne, Baraza la Shirikisho kwa kauli moja limeridhia kuyajumuisha majimbo ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia, kufuatia hatua kama hiyo iliyofanywa na Duma. Kinachofauta sasa ni kwamba nyaraka husika zipelekwe Ikulu ya Kremlin, kwa Rais Vladimir Putin kwa ajili ya kuzitia saini ikiwa ndio idhinisho kwa majimbo hayo manee, yenye ukubwa wa asilimia 18 ya eneo jumla lenye kutambulika kimataifa la Ukraine.

Urusi ilitangaza hatua ya kuyajumuisha maeneo hayo baada ya kuratibu kile walichokiita kura ya maoni katika maeneo wanayoyadhibiti. Mataifa ya Magharibi na serikali ya Kyiv yanasema zoezi hilo lilikiuka sheria za kimataifa, lilikuwa la shuruti na lisilo na uwakilishi.

Msimamo wa serikali ya Urusi kuhusu kura ya maoni

Sergey Lavrov ni waziri wa Mambo ya Nje ya Urusi."Uamuzi wa kuzikubali jamhuri za Donetsk na Luhansk za mikoa ya Zaporozhzhiya na Kherson katika Shirikisho la Urusi unatokana na matakwa ya kura ya maoni ya Septemba 23. Wakazi wa maeneo hayo walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa uhuru, kama yalivyothibitishwa na waangalizi wengi, wakiwemo wa kimataifa.

Rais Vladimir Putin wa UrusiPicha: Grigory Sysoyev/AP Photo/picture alliance

Pamoja na kupitia katika hatua za kibunge, lakini bado serikali ya Urusi haijafanya marekebisho ya mipaka mpiya ya mikoa hiyo mipya, ambayo sehemu kubwa bado ipo katika udhibiti wa jeshi la Ukraine. Kwa hivyo hajawa wazi kama Urusi itaweka mipaka yake yenyewe baada ya mchakato kamali wa kuyanyakua maeneo hayo utakamilika.

Jana Jumatatu, msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kremlin Dmitry Peskov alisema mashauriano yalikuwa yakiendelea kuhusu mipaka ya Mikoa ya Zaporizhzhia na Kherson. Kimsingi Urusi haijawa na udhibiti kamili ya mkoa wowote kati ya hiyo minne. Na katika uwanja wa mapambano jeshi la Ukraine limesema limeviteketeza vifaru 31 na mtambo wa kufyatulia roketi. Taarifa hiyo ya kamandi ya kijeshi ya kusini mwa Ukraine haitoa ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo.

Warusi zadi ya 200,000 wavuka mpaka na kuingia Kazakhstan

Katika hatua nyingine zaidi ya raia 200,000 wa Urusi wanaelezwa kuondoka nchini mwao na kuingia taifa jirani la Kazakhstan, tangu serikali ya Urusi itangaze uundwaji wa jeshi la nyongeza kwa amri ya rais katika jitihada yake ya kukabiliana na nguvu ya kijeshi nchini Ukraine.

Soma zaidi: Urusi yajiandaa kuyanyakua rasmi maeneo ya Ukraine

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kazakhastan, Marat Akhmetzhanov pasipo kutoa maelezo zaidi amesema idadi nyingine ya Warusi 147,000 imeondoka nchini humo tangu Septemba 21. Kadhalika ameongeza kuwa hadi wakati huu kuna maombi ya uraia ya Warusi 68.

Vyanzo: RTR/DPA

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW