Urusi kujitoa kwenye mkataba unaokataza majaribio ya nyuklia
25 Oktoba 2023Matangazo
Hiyo ni hatua ya mwisho kabla ya sheria hiyo kupelekwa kwa Rais Vladimir Putin kwa ajili ya kutia saini.
Baraza la Shirikisholiliidhinisha sheria hiyo kwa pamoja bila pingamizi kwa kura 156.
Soma pia:Urusi kwenye hatua za mwisho kujiondowa Mkataba wa Nyuklia
Mapema mwezi huu, Rais Putin aliwahimiza wabunge kufanya mabadiliko ili kuakisi msimamo wa Marekani ambayo ilitia saini mkataba huo lakini haikuidhinisha kikamilifumkataba wa marufuku dhidi ya majaribio ya silaha za nyuklia.
Urusi inasema haitarejelea majaribio ya nyuklia endapo Marekani nayo haitafanya.