1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal: Baraza la Katiba lachapisha orodha mpya ya wagombea

21 Februari 2024

Baraza la Katiba nchini Senegal limechapisha orodha mpya iliyofanyiwa madabadiliko ya wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi ujao uliocheleweshwa.

Maandamano nchini Senegal kulalamikia kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu
Maandamano nchini Senegal kulalamikia kuahirishwa kwa uchaguzi mkuuPicha: John Wessels/AFP

Jina la mgombea mmoja limeondolewa kwenye orodha hiyo mpya baada ya mgombea huyo Rose Wardini kutoka kambi ya upinzani kutangaza kujiondoa katika kinya'ng'anyiro hicho bila ya kuweka wazi sababu za kufanya hivyo.

Baraza la Katiba limesema wagombea kiti cha urais sasa wamebakia 19.

Wanasiasa vigogo wa upinzani ikiwemo mwenye ushawishi mkubwa na ambaye sasa yuko gerezani Ousmane Sonko pamoja na mtoto wa zamani wa Rais Abdoulaye Wade hawamo kwenye orodha hiyo.

Hata hivyo bado tarehe ya uchaguzi mpya haijaamuliwa.