Baraza la Mawaziri la Nigeria kuamua hatima ya Rais YarÁdua
23 Januari 2010Kiongozi huyo mwenye miaka 58 hakuonekana hadharani tangu mwezi wa Novemba alipokwenda Saudi Arabia kwa matibabu ya moyo. Jaji Dan Abutu amelitaka baraza la mawaziri kupitisha uamuzi wake kuhusu afya ya rais YarÁdua katika kipindi cha siku kumi na nne. Hatua hiyo inachukuliwa baada ya mbunge mmoja wa zamani kuishtaki serikali kuwa imekwenda kinyume na katiba ya nchi kwa kutomkabidhi madaraka kiongozi mwengine.
Mapema mwezi wa Desemba,baraza la mawaziri kwa kauli moja lilikubaliana kuwa hakuna sababu ya kumtaka Rais YarÁdua kujiuzulu. Mawaziri hao walipinga mito ya kumtaka ajiuzulu au kuthibitisha iwapo afya yake inamruhusu kubakia madarakani.
Baadhi ya wachambuzi wanasema,mawaziri wanasita kumpinga YarÁdua kwa sababu ya kuhofia kuwa watapoteza kazi zao ikiwa Makamu wa Rais Goodluck Jonathan atakabidhiwa madaraka.
Mwandishi:Martin,Prema/RTRE
Mhariri: Kitojo,Sekione