1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la mawaziri Ujerumani laidhinisha bajeti ya 2025

17 Julai 2024

Baraza la Mawaziri la Ujerumani limekamilisha bajeti ya mwaka 2025 baada ya wiki kadhaa za mabishano, na kuipeleka bungeni bajeti hiyo ya jumla ya euro bilioni 480 kwa uidhinishwaji.

Christian Lindner
Waziri wa fedha wa Ujerumani Christian LindnerPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance/dpa

Bajeti hiyo imekuwa mada kuu ya majadiliano kwa wiki kadhaa ndani serikali ya muungano ya Kansela Olaf Scholz. 

Bajeti hiyo ya euro bilioni 480.6, imepungua takriban bilioni 8 ikilinganishwa na mwaka huu.

Viongozi wa serikali ya Ujerumani hatimaye waafikiana kuhusu bajeti

Pendekezo la awali, ambalo lilikubaliwa na viongozi wa serikali ya muungano mapema mwezi huu, lilipingwa vikali na wakosoaji kwa madai kwamba halikuzingatia vya kutosha kuimarisha jeshi na kuchochea ukuaji.

Waziri wa Fedha Christian Lindner amepongeza makubaliano hayo na kuyataja kama "mwanzo wa mabadiliko ya kiuchumi" kwa Ujerumani.

Bajeti hiyo sasa ni lazima ipitishwe na wabunge, katika kura ambayo huenda ikafanyika mnamo Novemba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW