1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Mawaziri lajiuzulu Japan

Thelma Mwadzaya16 Septemba 2009

Waziri Mkuu wa Japan Taro Aso pamoja na baraza lote la mawaziri wamejiuzulu rasmi baada ya kushindwa katika uchaguzi wa kitaifa uliofanyika mwezi uliopita.

Waziri Mkuu wa Japan aliyejiuzulu Taro AsoPicha: AP

Hatua hiyo inaipa nafasi serikali mpya inayoongozwa na chama cha mrengo wa kati unaoegemea kushoto cha Demokratik kuingia rasmi madarakani.Hii ni mara ya kwanza chama cha Liberali cha Bwana Aso kimepoteza nafasi yake serikalini katika kipindi cha takriban miaka 50.Bunge hilo jipya linatarajiwa kumteua Yukiyo Hatoyama aliye kiongozi wa chama cha Demokratik kuwa Waziri mkuu mpya.