1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Seneti Kenya kuamua juu ya hatma ya Gachagua

Sylvia Mwehozi
17 Oktoba 2024

Baraza la Senate nchini Kenya jana Jumatano lilianza mchakato wa kusikiliza tuhuma zinalenga kumtimua naibu wa rais Rigathi Gachagua. Mwanasiasa huyo amekana madai yote akidai kuwa hoja ya kumtimua imechochewa kisiasa.

 Rigathi Gachagua
Naibu wa rais wa Kenya Rigathi GachaguaPicha: picture alliance / NurPhoto

Baraza la seneti nchini Kenya linatazamiwa kupiga kura leo iwapo litamtimua naibu wa rais Rigathi Gachagua katika sakata la kisiasa ambalo halijawahi kushuhudiwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Baraza la Seneti litatoa uamuzi wake leo katika siku ya pili ya kusikilizwa hoja ya kuondolewa madarakani kwa Gachagua, katika mchakato ulioanza jana Jumatano. Mchakato huo ulianzishwa baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbaliombi la mwanasiasa huyo aliyetaka hoja hiyo kuzuiwa na isiendelee kujadiliwa kwenye Baraza la Seneti. Wiki iliyopita, wabunge walipiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua kwa mashitaka 11, ikiwemo ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. 

Mwanasiasa huyo amekana madai yote akidai kuwa hoja ya kumtimua ilitokana na madai yaliyochochewa kisiasa. Endapo maseneta wasiopungua 45 kati ya 67 watapiga kura kuthibitisha mashtaka 11 yanayomuandama, basi naibu wa rais atatimuliwa.