1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Seneti Kenya kujadili hoja ya kuondolewa Gachagua

9 Oktoba 2024

Baraza la Seneti la Kenya linakutana kwa ajili ya kuanza kusikiliza hoja ya kuondolewa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Baraza la Seneti la Kenya kujadili hoja ya kuondolewa madarakani Rigathi Gachagua
Baraza la Seneti la Kenya kujadili hoja ya kuondolewa madarakani Rigathi GachaguaPicha: Andrew Kasuku/AP/picture alliance

Hoja hiyo inamtuhumu Gachagua kwa ufisadi, ukaidi, kuidhoofisha serikali na kuendesha siasa za migawanyiko ya kikabila, miongoni mwa mashtaka mengi ambayo ameyakanusha vikali.

Spika wa Baraza la Seneti, Amason Jeffah Kingi, amesema vikao vya kusikiliza hoja hiyo vimeanza saa tatu asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.

Baraza hilo lina siku 10 kukamilisha kesi hiyo na kufanya uamuzi kuhusu hoja hiyo, ambayo itahitaji kuungwa mkono na takribani theluthi mbili ya maseneta ili kuidhinishwa.

Iwapo ataondolewa, Gachagua atakuwa naibu rais wa kwanza kuondolewa madarakani kwa njia hiyo tangu hoja ya kuondolewa madarakani ilipoingizwa katika katiba ya Kenya iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW