1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Venezuela: Ripoti ya UN ni ya uongo

15 Agosti 2024

Baraza za uchaguzi la Venezuela linalokabiliwa na shinikizo kufuatia matokeo yaliyompa ushindi Rais Nicolas Maduro limeikosoa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na matokeo hayo likisema imegubikwa na uwongo.

Venezuela | Uchaguzi wa rais | Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro anakabiliwa na shinikizo sambamba na baraza la uchaguzi kufuatia matokeo ya uchaguzi yanayozozaniwa yaliyomrejesha madarakaniPicha: Matias Delacroix/AP Photo/picture alliance

Ripoti ya awali iliyoachapishwa siku ya Jumanne na jopo la wataalamu wa uchaguzi wa Umoja wa Maaifa iligundua kwamba CNE ilishindwa kutekeleza kikamilifu misingi ya uazi na uadilifu.

Baraza hilo, CNE lilitangaza ushindi wa Maduro kwa asilimia 52, bila ya kutoa mchanganuo. Matokeo hayo yamekuwa yakipingwa na upinzani, Marekani, Umoja wa Ulaya na baadhi ya mataifa ya Amerika ya Kusini.

CNE  jana Jumatano ilisema ripoti hiyo imejaa uongo na inakanganya na kusisitiza kwamba shambilizi la kigaidi la mtandaoni liliwazuia kutoa mchanganuo kamili wa matokeo.

Soma pia: UN: Watu 1,260 wamekamatwa Venezuela kufuatia vurugu za uchaguzi

Wizara ya mambo ya nje ya Venezuela pia imekataa ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Brazil na Colombia wajadili njia za kuisaidia Venezuela

Katika hatua nyingine, Rais wa Brazil na Colombia wamezungumza kwa njia ya simu na kuangazia namna wanavoweza kupata makubaliano ya kumaliza mgogoro nchini Venezuela siku ya Jumatano, hii ikiwa ni kulingana na Rais Luiz Inacio Lula da Silva.

Amesema "Nimezungumza kwa siku na Colombia, ili kujaribu kuona kama tunaweza kupata namna ya kusuluhisha matatizo ya nchini Venezuela, na kuona kama tunaweza kurejesha tena utulivu nchini humo."

Vikosi vya usalama vikipambana na waandamanaji katikka mji wa Caracas wanaopinga matokeo ya uchaguzi yaliyomrejesha madarakani Nicolas Maduro Picha: Matias Delacroix/AP/dpa/picture alliance

Mazungumzo hayo yaliwajumuisha kati ya Lula Rais Gustavo Petro wa Colombia, yalifikiwa baada ya Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador kujiondoa kwenye mkakati huo wa marais watatu kuelekea mzozo huo wa kisiasa nchini Venezuela, vyanzo viwili vimeiambia Reuters.

Brazil na Colombia wamekuwa wakiratibu juhudi zao za kidiplomasia katika kusuluhisha mzozo huo wa Venezuela ulioibuka tangu matokeo hayo ya baada ya uchaguzi wa Julai 28.

Lula na Petro pia wametolea wito mamlaka za Venezuela kuchapisha matokeo hayo kwa kina.

Rais Joe Biden pia aelezea wasiwasi juu ya hali nchini Venezuela

Mexico kwa upande wake imesisitiza kwamba mzozo huo wa baada ya uchaguzi unaweza kusuluhishwa na Venezuela mwenyewe. "Hili ni suala linalowahusu Wavenezuela na kile tunachotaka ni eneo hilo kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani.

Rais Joe Biden wa Marekani pia ameelzea mashaka juu ya hali inavyoendelea nchini VenezuelaPicha: Fernando Llano/picture alliance/AP-Carolina Cabral/Getty Images

Soma pia: Mwendesha mashitaka mkuu Venezuela afungua uchunguzi wa jinai dhidi ya viongozi wa upinzani

Pamoja na viongozi hao wa mataifa ya Amerika ya Kusini, Rais Joe Biden wa Marekani naye amezungumza na Rais wa Panam Jose Raul Mulino kwa njia ya simu, na kuelezea wasiwasi wao kuhusiana na udanganyifu mkubwa katika mchakato wa kuhesabu kura nchini Venezuela, Ikulu ya White House imesema.

Kiongozi wa zamani wa upinzani Enrique Marquez ambaye pia aliwahi kugombea dhidi ya Maduro na ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye CNE amesema siku ya Jumatano kwamba angeiomba ofisi ya mwendesha mashitaka kuanzisha uchunguzi wa jinai dhidi ya wafanyakazi wenzake wa zamani kwenye Baraza hilo la uchaguzi.

Soma pia:Upinzani Venezuela waitisha maandamano ya dunia Agosti 17