1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Baraza la UN laidhinisha uchunguzi wa uhalifu nchini Sudan

12 Oktoba 2023

Baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio linalofungua njia ya uchunguzi wa hali ya kiutu nchini Sudan.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu milioni 18 wanahitaji misaada nchini Sudan.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu milioni 18 wanahitaji misaada nchini Sudan.Picha: Marie-Helena Laurent/WFP/AP/picture alliance

Katika machafuko ya sasa nchini SUdan, jeshi na kikosi cha Dharura, RSF wamekuwa wakipambana kwa miezi sita iliyopita.

Mataifa 19 yalipiga kura kuunga mkono azimio hilo, 16 yakapinga na 12 hayakupiga kura.

Mwakilishi maalumu wa Marekani kwenye baraza hilo Michele Taylor amesema azimio hilo ni mwito wa kuchukua hatua kwa yale ambayo kila mmoja anakubali kuwa ni masuala muhimu kwa pande zinazopigana ili kuhitimisha ukatili na unyanyasaji mwingine, kusitisha mapigano na kuruhusu upitishjwaji salama wa haraka na usiozuiliwa wa misaada ya kiutu unaohitajika sana.

RSF imekanusha shutuma za watetezi wa haki kuwa iko nyuma yake mashambulizi dhidi ya raia, huku akisema wanajeshi wake watakaopatikana na makosa watafikishwa mahakamani

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW