1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Baraza la Usalama kukutana na waathirika wa vita vya Gaza

11 Desemba 2023

Mabalozi wa mataifa wanachama wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa wamekwenda Misri leo kukutana na raia wa Gaza walioathirika kutokana na vita vinavyoendelea kati ya kundi la wanamgambo la Hamas na Israel.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: David Dee Delgado/REUTERS

Ziara hiyo imekuja siku kadhaa bada ya Marekani kuzuia azimio la kutaka vita visitishwe.

Ziara hiyo ya siku moja isiyokuwa rasmi ilipangwa na Umoja wa Falme za kiarabu pamoja na Misri na imekuja katika wakati ambapo mgogoro wa kibinadamu umesambaa katika Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na vita.

Mabalozi kadhaa wakiwemo kutoka Urusi na Uingereza ni miongoni mwa waliokuwemo kwenye ziara hiyo.

Wametembelea hospitali ya El Arish iliyoko karibu na mpaka wa Rafah wa kuingia Gaza. Ufaransa na Marekani hazikuwakilishwa katika ziara hiyo.