1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Baraza la Usalama kupiga kura juu ya mzozo wa Israel-Gaza

18 Oktoba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapiga kura Jumatano juu ya Azimio lililoandaliwa na Brazil .

Azimio litakalopigiwa kura linalenga kushinikiza usitishaji mashambulizi mashambulizi ya israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas, ili misaada ifikishwe Gaza.
Azimio litakalopigiwa kura linalenga kushinikiza usitishaji mashambulizi mashambulizi ya israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas, ili misaada ifikishwe Gaza. Picha: Craig Ruttle/AP/picture alliance

Azimio hilo linataka kusitishwa kwa mzozo kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikishwa katika Ukanda wa Gaza.

Rasimu ya azimio hilo inaitaka Israel (lakini bila ya kuitaja jina) kubatilisha agizo lake kwa raia wa Gaza kuhamia kusini mwa eneo la Palestina.

Baraza hilo lenye nchi wanachama 15 lilitarajiwa kupiga kura hiyo siku ya Jumatatu, lakini iliahirishwa kwa muda wa saa 24 ili kuruhusu majadiliano.

Haijabainika wazi ikiwa Marekani ambayo ina kura ya turufu na pia mshirika wa karibu wa Israel itaruhusu azimio hilo kupitishwa.

Wanadiplomasia wamesema, baadaye, baraza hilo litajadili shambulizi katika hospitali ambalo limesababisha vifo vya mamia ya watu mjini Gaza. Hilo ni kufuatia ombi la Umoja wa Falme za Kiarabu na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW