1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Baraza la Usalama la UM kujadili vita vya Sudan

18 Novemba 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa Jumatatu kujadili rasimu ya azimio linalotaka kusitishwa mara moja kwa uhasama nchini Sudan.

Silaha ikiwa na bendera ya Sudan
Silaha ikiwa na bendera ya SudanPicha: Umit Bektas/REUTERS

Hayo yanajiri wakati ambapo vita kati ya majenerali wawili wanaohasimiana havionyeshi dalili zozote za kufikia kikomo.

Muswada huo ulioandaliwa na Uingereza na Sierra Leone, unatoa wito kwa wahusika "kusitisha uhasama mara moja na kushiriki kwa nia njema katika mazungumzo ya amani ili hatimaye kufikiwa mpango wa usitishwaji mapigano.

Soma pia: Watafiti wasema huenda vifo Sudan ni vingi zaidi ya vinavyoripotiwa

Sudan imeharibiwa na vita tangu Aprili mwaka 2023 kufuatia mapigano kati ya jeshi la la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye alichukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2021, na Kikosi cha RSF kinachoongozwa na naibu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW