1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN yaelezea kushtushwa na kuongezeka kwa ghasia Sudan

24 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeelezea "kushtushwa" na kuongezeka kwa ghasia nchini Sudan, siku moja baada ya kuripoti kuwa watu milioni saba wamekimbia makazi yao kutokana na mzozo huo

Shambulizi la kikosi cha RSF katika soko la mifugo la al-Fasher Kaskazini mwa Darfur mnamo Septemba 1, 2023
Shambulizi la kikosi cha RSF katika soko la mifugo la al-Fasher Kaskazini mwa DarfurPicha: AFP

Katika taarifa ya pamoja, baraza la usalama limelaani vikali mashambulizi yanayowalenga raia na kuenea kwa vita katika maeneo yenye idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani, wakimbizi kutoka nje na watu wanaotafuta hifadhi.

Wanachama wa baraza la usalama wameeleza kusikitishwa kwao juu ya kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini Sudan.

Soma pia: Jeshi la Sudan lasema vikosi vyake vimeondoka Wad Madan

Mbali na wakimbizi wa ndani milioni saba, Umoja wa Mataifa umesema, watu wengine milioni 1.5 wamekimbilia katika mataifa jirani.

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, ameeleza kwamba kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM takriban watu 300,000 wameukimbia mji wa Wad Madani katika jimbo la Al-Jazira. Hili ni wimbi jipya la wakimbizi wa ndani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW