1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Baraza la Usalama la UN lakutana kuijadili Ukraine

30 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali nchini Ukraine, baada ya nchi hiyo na waungaji wake mkono kuomba mkutano wa dharura kujadili mashambulizi ya makombora na droni ya Urusi

Majengo yalioharibiwa na droni ya Urusi iliyodunguliwa katika mji wa Odesa, Kusini mwa Ukraine mnamo Desemba 27, 2023
Majengo yalioharibiwa na droni ya Urusi iliyodunguliwaPicha: Nina Liashonok/Avalon/Photoshot/picture alliance

Mashambulizi hayo ya Urusi yamewauwa  raia 31 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 160, kulingana na maafisa, huku Poland ikisema kombora la Urusi lilirukia katika anga yake kabla ya kurejea Ukraine.

Soma pia:Watu 24 wauawa Ukraine katika wimbi jipya la mashambulizi

Baada ya kuanza kwa mkutano huo, wanachama wa baraza hilo Marekani, Ufaransa na Ungereza zililaani mashambulizi dhidi ya Ukraine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, pia alilaani mashambulizi hayo kwa mujibu wa msemaji wake Stephane Dujarric.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW