1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama la UN lalaani mapinduzi ya Niger

29 Julai 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali hatua ya kubadilishwa kwa serikali halali ya Niger kwa kukiuka katiba, na kutoa wito wa kuachiliwa huru mara moja kwa Rais wa nchi hiyo Mohammed Bazoum.

Moja ya mikutano ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Moja ya mikutano ya Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: ED JONES/AFP/Getty Images

Katika taarifa iliyokubaliwa kwa pamoja, baraza hilo lenye wanachama 15 lilisisitiza haja ya kumlinda Bazoum, familia yake na maafisa wa serikali yake.

Soma zaidi: Jenerali Abdourahamane Tiane ajitangaza kuwa kiongozi mpya Niger

Taarifa hiyo imesema kuwa wanachama wa baraza hilo wameelezea wasiwasi kuhusu athari mbaya za mapinduzi ya serikali kinyume cha katiba katika kanda hiyo, kuongezeka kwa shughuli za kigaidi na hali mbaya ya kijamii na kiuchumi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW