1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama latoa wito wa kusimamisha mapigano Sudan

24 Juni 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kusimamisha mapigano nchini Sudan na pia linataka raia walindwe.

New York | Eine Sitzung des Sicherheitsrats der Vereinten Nationen
Picha: ED JONES/AFP/Getty Images

Taarifa hiyo fupi kwa vyombo vya habari ilitolewa baada ya mashauriano ya faragha. Baraza hilo pia limetaka kuongezwa kwa misaada ya kibinadamu kwa Sudan na kwa nchi jirani. Pia limetoa wito wa kuwaunga mkono wafanyakazi wanaogawa misaada na linataka sheria za kimataifa ziheshimiwe.

Soma zaidi:Wasudan waendelea kushambuliana licha ya makubaliano

Sudanilitumbukia katika mzozo katikati ya mwezi Aprili baada ya miezi kadhaa ya kuongezeka mivutano iliyosababisha mapigano ya wazi kati ya majenerali mahasimu. Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa tangu kuanza kwa vita hivyo, watu milioni 2.8 nchini Sudan wamepatiwa misaada muhimu na shirika hilo.   

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW