1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Baraza la Usalama la UN lataka mjumbe maalum kwa Afghanistan

30 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotaka kuteuliwa kwa mjumbe maalum kwa Afghanistan ili kuongeza ushirikiano na nchi hiyo na viongozi wake wa Taliban

Msemaji wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan Bilal Karimi akizungumza wakati wa mahojiano maalum mjini Kabul mnamo Mei 26,2022
Msemaji wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan - Bilal Karimi Picha: Bilal Guler/AA/picture alliance

Hatua hiyo inafuatia ripoti huru ya tathmini iliyotolewa mnamo Novemba ambayo ilitaka ushirikiano zaidi na Afghanistan kufuatia kurejea madarakani kwa Taliban mnamo Agosti 2021.

Soma pia:Baraza la usalama la UN lashinikizwa kuingilia kati ukandamizaji wa wanawake unaozidi nchini Afghanistan

Azimio hilo linamtaka Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutaja mjumbe maalum wa kuendeleza mapendekezo ya ripoti hiyo huru, hasa kuhusu masuala ya kijinsia na haki za binadamu.

Azimio hilo lilipitishwa baada ya wanachama 13 wa baraza hilo la usalama kupiga kura ya kuliunga mkono, huku Urusi na China zikikosa kushiriki kura hiyo.

Soma pia:Taliban yaadhimisha miaka miwili tangu kurejea madarakani

Kabla ya kura hiyo, balozi wa Japan katika Umoja wa Mataifa Yamazaki Kazuyuki, alisema kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu na Japan zinaamini kwa dhati kwamba tathmini hiyo huru inatumika kama msingi bora wa mijadala inayofanyika na itakayofanyika.