1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Umoja wa Mataifa kujadili kusitishwa uhasama nchini Sudan

18 Novemba 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa leo, kujadili rasimu ya azimio linalotaka kusitishwa mara moja kwa uhasama nchini Sudan.

New York | Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajadili rasimu ya usitishwaji uhasama nchini SudanPicha: David Dee Delgado/REUTERS

Muswada huo ulioandaliwa na Uingereza na Sierra Leone, unatoa wito kwa wahusika "kusitisha uhasama mara moja na kushiriki kwa nia njema katika mazungumzo ya amani ili hatimaye kufikiwa mpango wa usitishwaji mapigano.

Sudan imeharibiwa na vita tangu Aprili mwaka 2023 kufuatia mapigano kati ya jeshi la la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye alichukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2021.

Kikosi cha RSF kinaongozwa na naibu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW