UN kupiga kura kuhusu kurejesha vikwazo dhidi ya Iran
19 Septemba 2025Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambazo zilitia saini mpango wa mwaka 2015 ulionuia kuizuia Tehran kumiliki silaha za nyuklia , wanadai kuwa Iran imevunja ahadi zake chini ya mkataba huo. China na Urusi zinapinga hatua ya kurejeshwa kwa vikwazo hivyo.
Lakini vyanzo vya kidiplomasia vinatarajia kuwa azimio hilo halitapata kura tisa zinazohitajika ili kudumisha hali ya sasa na kwamba vikwazo hivyo vinatarajiwa kuanzishwa tena. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema vikwazo hivyo vinatarajiwa kurejeshwa mwishoni mwa mwezi huu.
Tanbihi ya Mhariri: Makala hii awali ilijumuisha picha kutoka shirika la SalamPix. Iliondolewa tarehe 12 Machi 2026 baada ya Picture Alliance na Imago kutuarifu kuwa walikuwa wanaondoa picha za SalamPix kutokana na wasiwasi kuhusu chanzo chake na uwezekano wa kuwa zimehaririwa.