Baraza la Usalama la UN lagawanyika kuhusu Gaza
15 Novemba 2025
Matangazo
Wajumbe wamesema kura hiyo inaweza kufanyika mapema wiki ijayo. Rasimu ya Marekani inalenga kuwezesha utekelezaji wa mpango wa amani wa Rais Donald Trump kwa eneo zima la Mashariki ya Kati.
Kwa upande wake, Urusi imewasilisha azimio lake, ambalo linajumuisha kuitambua Palestina kama taifa, huku China ikiashiria kuwa tayari kuiunga mkono rasimu ya Urusi.
Misri, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Pakistan, Saudi Arabia, Jordan na Uturuki zimeunga mkono hadharani rasimu ya Marekani.
Urusi, China na Marekani zote zinashikilia kura ya turufu katika baraza hilo, hii ikimaanisha kuwa azimio lolote wanalolipinga haliwezi kupitishwa.