1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Baraza la Usalama la UN laongeza vikwazo vya silaha Haiti

19 Oktoba 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja kuongeza vikwazo vya silaha dhidi ya Haiti, wakati taifa hilo likijitahidi kujiimarisha na kuchukuwa udhibiti dhidi ya magenge ya uhalifu.

Kiongozi wa muungano wa makundi ya uhalifu nchini Haiti Jimmy "Barbecue" Cherizier afyatua risasi hewani baada ya mkutano na waandishi wa habari mjini Port-au-Prince, Haiti mnamo Machi 11, 2024
Kiongozi wa muungano wa makundi ya uhalifu nchini Haiti Jimmy "Barbecue" CherizierPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Wanachama wote 15 wa Baraza hilo la Umoja wa Mataifa walipigia kura azimio hilo, ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuzuia usafirishaji wa silaha za aina yoyote kuingizwa Haiti.

Vikwazo vilivyowekwa awali, vililenga tu silaha ndogo ndogo na risasi.

Azimio liliwasilishwa na Ecuador na Marekani

Azimio hilo lililowasilishwa jana na Ecuador na Marekani, pia linajumuisha kuongezwa muda wa mwaka mmoja kwa kamati ya kufuatilia vikwazo dhidi ya baadhi ya raia wa Haiti.

Mwakilishi wa Marekani, Dorothy Shea, aliliambia Baraza hilo kwamba hali nchini Haitibado ni mbaya mno.

Shea ameongeza kuwa Marekani bado ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na kibinadamu nchini Haiti na kwamba watu wengi bado wanaendelea kuteseka kutokana na vurugu hizo zinazoendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW