1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa MONUSCO kusalia Kongo kwa mwaka mmoja

21 Desemba 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja ya kurejesha mamlaka ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mwaka mmoja.

DR Kongo | UN MONUSCO
Mwanajeshi wa MONUSCO huko karibu na Kibumba, kaskazini mwa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Januari 28, 2022. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Kongo unasaidia vita dhidi ya waasi kwa zaidi ya miongo miwili.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa limerejesha mamlaka ya kikosi hicho kwa kipindi hicho hata ikiwa ujumbe huo utajiondoa hatua kwa hatua kufuatia ombi la Kinshasa.

Azimio hilo lililopitishwa Ijumaa linasema Baraza hilo linaunga mkono "kujiondoa kwa utaratibu kwa ujumbe wa MONUSCO kulingana na hali ya usalama ya ndani."

Azimio hilo pia limeeleza wasiwasi wake juu ya "kuendelea kwa ghasia mashariki mwa Kongo na mvutano unaoendelea kati yake na Rwanda.

MONUSCO tayari imekamilisha mchakato wa kuondoka huko Kivu Kusini baada ya kufunga ofisi yake mwishoni mwa Juni, lakini wanajeshi wake bado wako Ituri na Kivu Kaskazini.

MONUSCO ina wanajeshi na polisi wapatao 16,000.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW