1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama lahofia "kutanuka ghasia" Kongo Mashariki

13 Februari 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatiwa hofu na "kuongezeka kwa hali ya machafuko" mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kulaani mashambulizi ya hivi karibuni ya kundi la waasi wa M23 karibu na Goma.

Kikao cha Baraza la Usalama kuhusu Afghanistan
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kikaoniPicha: Eskinder Debebe/UN Photo/picture alliance/Xinhua News Agency

Wajumbe wa baraza hilo waliokutana jana Jumatatu, wamerejea matamshi yao ya kuyalaumu makundi ya wapiganaji yanayoendesha operesheni zao nchini humo kuwa chanzo cha kudodora hali ya usalama upande wa mashariki.

Wamesisitiza msimamo wao wa kuiunga mkono Kongo katika kulinda uhuru wake na kuheshimiwa hadhi ya mipaka ya taifa hilo.

Serikali ya Kongo, Umoja wa Mataifa na nchi za magharibi zinaituhumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 kwa dhamira ya kudhibiti utajiri wa madini mashariki mwa Kongo.

Kundi hilo la waasi limeyakamata maeneo makubwa mashariki mwa Kongo tangu lilipozukla tena mwaka 2021 na sasa linatishia kuuchukua kwa mara nyingine mji wa kimkakati wa Goma.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW