1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama laonya dhidi ya hali mbaya Kongo

21 Juni 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonya kuhusu harakati za makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiwa ni pamoja na mapigano ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

DR Kongo Goma 2024
Wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Baraza hilo limesema mashambulizi ya waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) yamekuwa yakiongezeka kwenye eneo hilo.

Vile vile limelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya M23, ambayo vyanzo vya ndani vinasema yalikuwa ya umwagaji mkubwa wa damu.

Soma zaidi: AU walaani mauaji ya watu wengi nchini DR Congo

Mashambulizi ya wiki iliyopita huko Kanyabayonga, mji muhimu katika eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye machafuko, yaliwafanya watu 350,000 kupoteza makaazi yao.

Ingawa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikulitaja bayana jina la Rwanda, lakini lililaani kile ilichokiita msaada wa kijeshi wa kigeni unaotolewa kwa waasi na kutoa wito wa kuondolewa mara moja kwa vikosi vyote vya kigeni.

Rwanda imekuwa mara kadhaa ikikanusha kuwaunga mkono waasi wa M23.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW