Baraza la wawakilishi lakutana visiwani Zanzibar
20 Januari 2010Kikao hicho kimeanza leo, kutaka kuwasilisha hoja ya kibinafsi ikilitaka baraza liyaimarishe maafikiano ya maridhiano yaliofikiwa karibuni baina ya Rais wa Zanzibar, Amani Karume, na katibu mkuu wa Chama cha CUf, Seif Shariff Hamad. Wachunguzi wa mambo wanaiona hoja hiyo itakuwa ni kama utangulizi wa kutaka vifungu fulani vya katiba ya sasa ya Zanzibar vibadilishwe, na huenda kuweza kurefusha muda wa kubakia madarakani Rais Karume baada ya kipindi chake cha sasa cha hadi Oktoba mwaka huu na pia kuwa na serekali ya kitaifa. Hata hivyo, waziri kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, aliwahi kusema kwamba hakuna wakati wa kutosha kufanya mabadiliko ya katiba kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanywa Oktoba mwaka huu.
Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu alasiri ya leo na Abubakar Khamis Bakary, na akamuuliza kama kweli hoja yake hiyo inataka uchaguzi wa Zanzibar uahirishwe...
Mtayarishaji: Othman Miraji
Mhariri:Aboubakary Liongo