SiasaMarekani
Bunge la Marekani lapitisha muswada wa ukomo wa kukopa
1 Juni 2023Matangazo
Kura hiyo ni hatua muhimu katika kuzuia hatari ya serikali ya nchi hiyo kushindwa kuyalipa madeni yake, hali ambayo inaweza kuiyumbisha nchi hiyo.
Rais Joe Biden amesema makubaliano hayo ni habari njema kwa watu wa Marekani na kwa uchumi wao. Sheria ya uwajibikaji wa kibajeti ilihitaji wingi mdogo wa kura katika baraza hilo la wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Republican.
Soma pia: Biden na Warepublican wakubaliana ukomo wa Deni la Taifa
Baada ya hapo muswada huo utapelekwa katika baraza la seneti, kabla ya kuwasilishwa kwenye meza ya rais ili usainiwe kuwa sheria.